DAR ES SALAM:

 
Viongozi wawili kati ya makasisi 36 wa Kiislamu maarufu kwa jina la Sheikh wa Uamsho Farid Hadi Ahmed na Mselemu Ali Mselemu ambao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya ugaidi wameachiliwa.
 
Sheikh Farid na wenzake ambao walikuwa kizuizini tangu mwaka 2014 kutokana na mashtaka ya ugaidi waliachiliwa jana baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), kuwafungulia mashtaka.