LAMU HADI NAIROBI

LAMU
Leo Mhe. Waziri Najib Balala alikuwa miongoni mwa waheshimiwa kadhaa waliotuwa katika uwanja wa ndege wa Manda, Lamu kwa sherehe ya uzinduzi wa safari za ndege za moja kwa moja za Jambojet kutoka uwanja wa ndege wa JKIA wa Nairobi hadi Lamu.
Waziri pia alizindua rasmi chapa ya ndege ya MagicalKenya na Fly Jambojet, wakati wa safari ya kwanza ya moja kwa moja kutoka Nairobi kwenda Lamu.