UNGUJA:

Serikali ya Zanzibar imeanzisha mfumo wa kutoa huduma (EMR) ambapo mgonjwa anafuatiliwa kila hatua kuanzia anapotoka kwa daktari, kuchukua dawa hadi kurejea nyumbani.
 
Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Juni 16, 2021 na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui.
 
Amebainisha kuwa wizara inaendelea na mikakati ya kidigitali ya afya wenye lengo la kuanzisha mifumo wenye ubora kwa ajili ya kuimarisha utoaji huduma.